Watu 11 wafariki kwenye ajali Nakuru

  • | Citizen TV
    1,862 views

    Watu 11 wamefariki kufuatia ajali ya barabarani iliyotokea katika eneo la Sobea, kaunti ya Nakuru kwenye barabara ya Nakuru kuelekea Eldoret mapema hii leo. Watu wengine kadhaa waliojeruhiwa wanaendelea kutibiwa katika hospitali ya Nakuru huku maafisa wa usalama wakichunguza kiini cha ajali hiyo iliyohusisha gari la abiria na trela.