Watu 8 wafariki kwenye ajali barabarani eneo la mlima Kiu kwenye barabara ya Mombasa-Naiorobi

  • | Citizen TV
    630 views

    Watu wanane wamefariki papo kwa hapo na wengine kupata majeraha baada ya matatu waliokuwa wakisafiria kugongana ana kwa ana na trela katika eneo la mlima Kiu kwenye barabara kuu ya Mombasa kuelekea Nairobi usiku wa kuamkia leo.

    kulingana na Kamanda wa polisi wa Mukaa kaunti ya makueni , Barbanas Ng’eno, japo kulikuwa na mvua nyingi kwenye eneo hilo, kuna uwezekano mkubwa mmoja wa madereva hakuzingatia sheria za barabarani kwenye eneo hilo ambalo ni hatari. Matatu hiyo ilikuwa na abiria kumi na sita ilitoka eneo la Loitoktok Nairobi . Miili ya waliofariki inahifadhiwa katika hospitai ya KIlungu.