Watu 8 wamefariki kufuatia ajali ya barabarani eneo la Ngata, Nakuru

  • | Citizen TV
    5,667 views

    Watu wanane wamefariki baada ya matatu walimokuwa kugongana na Trela katika barabara kuu ya Nakuru-Eldoret mapema leo alfajiri Ajali hiyo iliyotokea eneo la Ngata mwendo wa saa tisa asubuhi ilihusisha matatu iliyokuwa ikilekea upande wa Nakuru na trela lililokuwa likitoka upande wa Eldoret. Waliojeruhiwa walikimbizwa hadi hospitali ya Nakuru kwa matibabu. Walioshuhudia walizungumzia matukio kabla na wakati wa ajali hiyo