Watu wa Gaza walazimika kula nyama ya kasa kutokana na njaa

  • | BBC Swahili
    4,945 views
    Baadhi ya raia huko Gaza wanalazimika kula nyama ya kasa wa baharini walioko katika hatari ya kutoweka kwa sababu hawana chanzo kingine cha protini. Maelfu kwa maelfu ya wakazi wasiokuwa na makazi katika Ukanda wa Gaza wanahisi tishio la njaa kuwa karibu. Hii inatokea wakati ambapo Israel imeendelea kufunga mipaka kwa takriban miezi miwili, ikizuia kuingia kwa chakula, dawa, au hata maji safi ya kunywa. Israel inadai kuwa inazingatia sheria za kimataifa na hakuna uhaba wa misaada. #bbcswahili #Gaza #Israel Subscribe kupata video motomoto kila siku kutoka BBC Idhaa ya Kiswahili https://www.youtube.com/channel/UCoerKKIKIMlDYaVFSTlsWGw