Watu watatu wafariki mlolongo kaunti ya Machakos

  • | Citizen TV
    5,214 views

    Watu watatu wamepoteza maisha yao katika eneo la Mlolongo Kaunti ya Machakos kufuatia machafuko yaliyozuka wakati wa maandamano ya leo. Watatu hao waliuawa kwa kupigwa risasi huku wengine wakijeruhiwa katika rabsha kati ya polisi na waandamanaji zilizoendelea kwa zaidi ya saa sita.