Watu watatu wauawa katika shambulizi la kijangili katika kata ya Rugus, Baringo kusini.

  • | KBC Video
    31 views

    Watu watatu wameuawa katika shambulizi linaloshukiwa kuwa la kijangili katika kata ya Rugus, Baringo kusini. Watatu hao walikuwa malishoni walipovamiwa na kupigwa risasi. Mmoja wao alifanikiwa kutoroka bila kujeruhiwa. Kamanda wa Polisi katika kaunti ya Baringo, Julius Kiragu amesema vikosi vya usalama vinashirikiana ili kutokomeza visa vya ujangili kwenye eneo hilo. Viongozi wa eneo hilo wamelaani kisa hicho wakitaka serikali kuwakamata waliotekeleza shambulizi hilo na kuhakikisha mashambulizi ya aina hio yanafikia kikomo.

    Connect with KBC Online; Subscribe to our channel: https://t.ly/86BKN Follow us on Twitter: https://twitter.com/KBCChannel1 Find us on Facebook: https://www.facebook.com/kbcchannel1tv Check our website: https://www.kbc.co.ke/

    #KBCchannel1 #Kenya #News