- 3,962 viewsDuration: 2:33Watu wawili wamekamatwa kufuatia vurugu zilizoshuhudiwa eneo la Nembure, Kaunti ya Embu, na kusababisha vifo vya watu wawili. Haya yamejiri huku Mbunge wa Manyatta, Gitonga Mukunji, akikwepa mtego wa polisi wa kumkamata nyumbani kwake Mutunduri. Mukunji, aliyehudhuria ibada ya Jumapili Mbeere Kusini, amesisitiza kuwa hatishwi na hatua ya serikali ya kutaka kumkamata, huku akikanusha kuhusika na vurugu hizo. Gatete Njoroge anatuarifu.