Wauguzi kaunti ya Laikipia waendeleza mgomo kwa siku nne sasa

  • | Citizen TV
    219 views

    Wauguzi katika hospitali za rufaa za Nanyuki na Nyahururu wameendelea na mgomo wao kwa siku ya nne sasa, wakishinikiza kuajiriwa kwa kandarasi ya kudumu, kupandishwa vyeo, bima bora ya afya na kuajiriwa kwa wauguzi zaidi. Katika hospitali ya rufaa ya Nyahururu, wauguzi waliowasilisha malalamishi yao katika afisi za serikali waliapa kutorejea kazini hadi pale matakwa yao yatakaposhughulikiwa.