- 3,585 viewsDuration: 1:11Watu waliopona ugonjwa wa Ebola aina ya Bundibugyo wanatoa matumaini mapya kwa wahudumu wa afya na timu nyingine zinazopambana kudhibiti mlipuko huo. Hata hivyo, WHO inaeleza kuwa juhudi za kukabiliana na ugonjwa huo bado hazijafikia kiwango kinachohitajika ili kuutokomeza kikamilifu. DRC ni moja ya maeneo yaliyoathirika zaidi, hususan jimbo la Ituri kaskazini mashariki mwa nchi hiyo. BBC ilitembelea eneo hilo na kuripoti kutoka mji wa Mongbwalu, ambao ni mmoja wa vituo vitatu vikuu vya mlipuko huo wa Ebola. Subscribe kupata video motomoto kila siku kutoka BBC Idhaa ya Kiswahili https://www.youtube.com/channel/UCoerKKIKIMlDYaVFSTlsWGw