Wawekezaji wadai kulaghaiwa mabilioni ya pesa Eldoret

  • | Citizen TV
    3,622 views

    Mamia ya wakazi wa Eldoret kaunti ya Uasin Gishu wanalilia haki baada ya kulaghaiwa mamilioni ya pesa na kampuni moja ya uwekezaji. Waathiriwa wanasema kuwa mmiliki wa kampuni ya Springmark aliwaahidi kuwa watapata faida ya riba ya hadi asilimi 18 kwa mwezi wakiwekeza pesa zao . Cha kushangaza ni kuwa waliolaghaiwa ni wasomi,mameneja wa benki tofauti ,maafisa wa polisi , mawakili na viongozi wa makanisa wakiwemo maaskofu miongoni mwa wengine.