Wazaliwa wa Arusha tunapenda pikipiki

  • | BBC Swahili
    773 views
    Umoja wa vijana waendesha pikipiki kwa ajili ya mchezo katika jiji la Arusha nchini Tanzania wamenuia kubadili sifa mbaya wanazopewa wandesha pikipiki kwa kuonesha fursa zitokanazo na mchezo huo badala ya kufanya uhalifu. Pikipiki maarufu kama boda boda nchini Tanzania zimerahisisha kwa kiasi kikubwa shughuli za usafirishaji wa abiria na vifurishi hasa kwenye miji yenye msongamano kama Dar es salaam na maeneo ya vijijini ambako miundombini ni mibovu. Lakini takwimu zinaonesha kati ya mwaka 2022 na 2024 watu zaidi ya 10000 wamepoteza maisha kutokana na ajali zilizosababishwa na bodaboda. Mwandishi wa BBC @eagansalla_gifted_sounds akiwa Jijini Arusha alituandalia taarifa hii #bbcswahili #tanzania #bodaboda Subscribe kupata video motomoto kila siku kutoka BBC Idhaa ya Kiswahili https://www.youtube.com/channel/UCoerKKIKIMlDYaVFSTlsWGw