- 1,622 viewsDuration: 1:39Wazee wa jamii ya waswahili kaunti ya Mombasa wamelalamikia kuachwa nje katika masuala ya kitaifa na ya kaunti. Wakizungumza katika mtaa wa old town, wazee hao wanadai vijana kutoka jamii hiyo wanatengwa kwenye nafasi za kazi, suala ambalo wanadai linachangia kuwepo kwa magenge ya wahalifu. Sasa wanataka serikali kuu na ile ya kaunti kuhakikisha vijana wamepata ajira ili kukabiliana na matatizo yanayowakumba.