Waziri Nakhumicha ahojiwa na kamati ya Afya bungeni kuhusu saga ya NHIF

  • | Citizen TV
    90 views

    Waziri wa Afya Susan Nakhumicha amekiri kuwepo kwa watu wanaohusika na ubadhirifu wa fedha katika sekta ya Afya, akiahidi kupambana na wanaohusika. Waziri nakhumicha ameiambia kamati ya bunge kuhusu Afya kuwa, ripoti za baadhi ya hospitali kushirikiana kuwaibia wakenya kupitia malipo ya NHIF ni za aibu, akiwaonya wahusika kuwa siku zao arobaine zimefika. Nakhumicha akikiri mbele ya wabunge kuwa ripoti zilizojitokeza ni aibu kwake na wizara nzima ya Afya. Tayari maafisa wasimamizi wa matawi ya NHIF yaliyohusishwa na sakata hii wamesimamishwa kazi kutoa nafasi ya uchunguzi.