- 101 viewsDuration: 1:56Waziri wa kilimo Mutahi Kagwe amesitisha utoaji wa leseni za uagizaji wa sukari, akisema kuwa viwanda vya humu nchini vimezalisha sukari ya kutosha. Agizo hilo linajiri siku chache baada ya wadau katika sekta hiyo kulalamikia ongezeko la sukari ya magendo. Akizungumza baada ya mkutano na wakulima wa miwa, Kagwe pia amesema atahakikisha deni la shilingi milioni mbili kwa wakulima wa miwa limelipwa