Waziri wa usalama Kindiki atarajiwa kufika mbele ya kamati ya bunge kuhusu usalama

  • | Citizen TV
    227 views

    Hayo yakijiri, waziri wa usalama Profesa Kithure Kindiki leo anafika mbele ya kamati ya bunge kuhusu usalama, kuhusiana na utata wa kupandishwa vyeo kwa maafisa wa polisi. Waziri Kindiki anatarajiwa bungeni huku utata kati ya tume ya huduma za polisi na Inspekta Mkuu wa Polisi ukiendelea, kuhusiana na kupandishwa vyeo kwa maafisa 500 wa polisi. Mzozo huu umeendelea kuvutia hisia kutoka kwa wadau mbalimbali, wapunde zaidi wakiwa mawakili chini ya chama cha mawakili nchini LSK, wanaotaka mzozo huo kutatuliwa mara moja.