Waziri wa Usalama Kipchumba Murkomen asisitiza Gachagua aandikishe taarifa kwa DCI

  • | Citizen TV
    1,949 views

    Waziri wa usalama Kipchumba Murkomen amesisitiza kuwa aliyekuwa Naibu Rais Rigathi Gachagua lazima aandikishe taarifa kwa DCI kuhusiana na matamshi yake kuhusu mazungumzo na kundi haramu la Al Shabaab. Murkomen ambaye yuko katika kaunti ya Narok kwa mikutano ya Jukwaa la Usalama amemkashifu Gachagua kwa kutumia jukwaa la kimataifa kueneza propaganda dhidi ya taifa la Kenya na maafisa wa usalama.