Skip to main content
Skip to main content

Wito watolewa serikalini kuimarisha teknolojia ya kisasa

  • | Citizen TV
    150 views
    Duration: 1:39
    Wito umetolewa kwa serikali kuimarisha na kuboresha teknolojia ya kisasa katika sehemu za mashinani ili kusaidia vijana kuendeleza shughuli mbalimbali za kidiJitali, kama vile masomo na biashara za mtandaoni. Haya yanajiri wakati ambapo matumizi ya mifumo ya kidijitali, hasa teknolojia ya Akili unde yameshika kasi ulimwenguni kote. Hatua hiyo itasaidia kupiga jeki maisha ya vijana maeneo ya vijijini. Wito huo umetolewa na wafanyibiashara wa teknolojia Kaunti ya Elgeyo Marakwet ambao wamesisitiza haja ya serikali kuweka kipaumbele uboreshaji wa miundombinu ya teknolojia kwa minajili ya kuwainua vijana. Wakati huo huo, vijana katika kaunti hiyo wamehimizwa kukumbatia masomo na matumizi ya teknolojia ya kisasa ili kuhakikisha wameunganishwa vyema na mtandao kwa lengo la kuboresha maisha yao.