- 361 viewsDuration: 2:16Wizara ya Afya imetia saini mkataba na kaunti tatu za Nakuru, Garissa na Mombasa wa kutoa huduma maalum za ugonjwa wa saratani kwa wakazi wa kaunti hizo. Makubaliano hayo yatahakikisha vituo vya kutoa matibabu ya saratani vinafanya kazi kama vinavyofaa. Waziri wa Afya Aden Duale na magavana wa kaunti hizo tatu walishuhudia makubaliano hayo yatakayohusisha serikali kuu kutoa ufadhili wa mitambo ya saratani na kuhakikisha inafanya kazi. Serikali inapanga kufungua vituo kama hivyo katika kaunti zingine tano hivi karibuni.