Wizara ya Afya yalenga kutathmini vituo 15,000 vya umma na vya kibinafsi ili kuboresha utoaji huduma

  • | Citizen TV
    336 views

    Wizara ya afya imeanza rasmi mchakato wa kufanya sensa katika vituo mbalimbali vya afya ili kubaini mapungufu yaliyo kwenye sekta hiyo. Zoezi hilo linatarajiwa kuendelea kwa kipindi cha wiki mbili likilenga vituo 15000 vya umma na vya kibinafsi. Akizungumza wakati wa uzinduzi wa sensa hiyo ya vituo vya afya, waziri wa afya Susan Nakhumicha amesema kwamba takwimu zitakazojumuishwa kutokana na zoezi hilo zitasaidia wizara kubaini namna ya kuimarisha utoaji huduma katika vituo mbalimbali vya afya.