Zaidi ya familia 100 zimeathirika na mafuriko ya mto Sabwani, serikali yaagiza kuhama mara moja

  • | Citizen TV
    329 views

    Zaidi ya familia 100 katika eneo la Namanjalala, eneo bunge la Kwanza, Kaunti ya Trans Nzoia, zimewachwa bila makao baada ya mto Sabwani kuvunja kingo zake kufuatia mvua kubwa inayonyesha eneo hilo. Aidha mashamba yamesombwa na maji huku baadhi ya wagonjwa wakikosa hata njia za kufika hospitalini.