Zaidi ya wakaazi 600 wafaidika na huduma za matibabu ya macho eneo la Matuga, Kwale

  • | Citizen TV
    124 views

    Zaidi ya wakaazi mia sita wamepokea matibabu ya macho bila malipo katika eneo la Waa huko Matuga kaunti ya Kwale. Kambi hiyo ya matibabu iliyoandaliwa kwa ushirikiano wa wakfu wa Rashid Abdalla Super Cup, Saturday Club Mombasa na Mombasa Eye Hospital & Laser Centre imefanyika katika shule ya msingi ya Waa. Madaktari walikua wakikagua magonjwa ya macho yakiwemo mtoto wa jicho, Glaucoma na kutoona vema, huku ikisemekana visa vya ugonjwa wa Glaucoma au presha ya macho vinaongezeka. Lawrence Ng'ang'a anaarifu zaidi kutoka Kwale.