- 12,434 viewsDuration: 5:50Zhang Zhidong, anayejulikana pia kama "Brother Wang" alihitimu chuo kikuu kinachoheshimika zaidi nchini China. Aliwasili nchini Mexico akiwa na umri wa kati ya miaka ya ishirini, na kwa haraka akajifunza jinsi ya kujenga mahusiano na yeyote aliyekuwa na mamlaka makubwa—iwe ni viongozi wa serikali za mitaa au wahusika wa ulimwengu wa uhalifu. Anatuhumiwa kujenga mtandao mkubwa wa uhalifu uliomfanya kuwa kiungo muhimu kati ya viwanda vya kemikali vya China na magenge ya dawa za kulevya ya Mexico yaliyokuwa yakisambaza fentanyl kwa wingi kwenda Marekani. Wanachama wa magenge hayo nchini Mexico walimuita "El Rey" (Mfalme), wakimaanisha Mfalme wa Fentanyl, au "Número Uno" (Namba Moja), au kwa jina lake la utani "Brother Wang". Kwa sasa, anashikiliwa nchini Marekani akishtakiwa kwa makosa ya kusafirisha na kusambaza dawa za kulevya. BBC imechunguza kwa kina safari yake ya kupanda hadi kileleni na baadaye kuanguka, kwa kuzungumza na wanachama wa magenge ya dawa za kulevya wanaodai walishuhudia ushawishi wake moja kwa moja, pamoja na watafiti ambao wametumia miaka mingi kufuatilia mtandao wa usambazaji wa fentanyl. #bbcswahili #mexico #fentanyl Subscribe kupata video motomoto kila siku kutoka BBC Idhaa ya Kiswahili https://www.youtube.com/channel/UCoerKKIKIMlDYaVFSTlsWGw