IMF yaeleza ufadhili wa urekebishaji na upunguzaji athari za mabadiliko ya hali ya hewa

  • | VOA Swahili
    278 views
    Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Kimataifa la Fedha IMF, Kristalina Georgieva yuko nchini Rwanda kwa ziara ya siku tatu. Akiwa mjini Kigali amekutana na mawaziri wa fedha pamoja na magavana wa benki kuu za Rwanda, Uganda, Kenya na Sudan Kusini. Sikiliza nasaha zake kwa nchi za Kiafrika: "Kwa kifupi hakuna pesa za umma za kutosha kufadhili hatua za kurekebisha na kupunguza athari za mabadiliko ya hali ya hewa. Tunazungumzia trilioni ambazo ni muhimu na tunajadili mabilioni ya fedha zilizopo. Bila ya kutumia mabilioni kutengeneza mazingira mazuri kwa uwekezaji binafsi, hatuwezi kufikia, hatutafika popote. Wakati tumekaa katika chumba hiki sisi bado tumegawanyika, na nakiri, hivi ndivyo ilivyo. Benki ya Dunia inafanya hiki, Benki ya Maendeleo ya Afrika inafanya kile, kila mmoja ana mradi, yote hiyo ni mizuri sana. Lakini haisongi mbele," #imf #shirikalafedhalakimataifa #mkurugenzimkuu #kristalinageorgieva #kigali #rwanda #magavana #mawaziriwafedha #voa #voaswahili #dunianileo #benkiyadunia #benkiyamaendeleoyaafrika - - - - - #VOASwahili Sauti ya Amerika - Idhaa ya Kiswahili inawafikia zaidi ya watu milioni 100 wanaotembelea tovuti, mitandao ya kijamii, radio na televisheni zetu. Tunawasilisha maudhui kuhusu Afrika Mashariki na Kati kwa nchi takriban 11 huko Afrika na wale walioko ughaibuni na kwingineko duniani. Vipindi vyetu vimejikita katika maudhui mbalimbali ikiwemo habari, vijana, wanawake, siasa, sayansi, teknolojia, afya, biashara, michezo, muziki na burudani na pia tunawashirikisha wasikilizaji wetu.