- 6,178 viewsDuration: 3:33Maelfu ya wakenya walimiminika eneo la pwani kwa sherehe za krismasi kwenye fukwe za baharini, mikahawani na kwenye mabustani. Kando na kuongelea,wengi walijituliza kwa vyakula vitamu vya uswahilini huku wengine wakipunga upepo wa bahari. Na kama anavyoarifu francis mtalaki wadau katika sekta ya utalii wanahimiza doria ya usalama kuendelea ili kuwavutia watalii zaidi, shamrashamra za mwaka mpya zikianza.