- 6,072 viewsDuration: 48sTimu ya pamoja ya wapiga mbizi kutoka kaunti za Bomet na Narok ilifaulu kuuopoa mwili wa mwanume wa aliyezama kwenye bwawa la Chesonoi huko Ololmasani, Kaunti ya Narok. Inaarifiwa kuwa Weldon Kipng'etich mwenye umri wa miaka 21, alizama na kufa maji alipokuwa akiongelea katika bwawa hilo hapo jana. Kwa mujibu wa meneja wa idara ya maaafa kaunti ya Bomet Stanley Mutai, mwili wa marehemu ulipelekwa katika makafani ya hospitali ya Kapkatet. Vijana na umma kwa ujumla wameonywa kuwa waangalifu na kusherehekea sikukuu za krismasi na mwaka mpya kwa tahadhari hasa karibu na vyanzo vikubwa vya maji.