Skip to main content
Skip to main content

Mbunge wa Saboti Caleb Amisi ataka serikali kutafutia wafungwa kazi baada ya kuachiliwa

  • | Citizen TV
    1,328 views
    Duration: 1:23
    Mbunge wa Saboti Caleb Amisi, amesema atawasilisha mswada bungeni wa kuishinikiza serikali kuwapatia ajira wafungwa wanaoachiliwa huru baada ya kupata ujuzi mbalimbali wakiwa magerezani. Akizungumza wakati wa hafla ya kuwapa zawadi za Krismasi kwa wafungwa katika magereza matatu mjini Kitale, Amisi amesema mpango huo utasaidia kupunguza ukosefu wa ajira na kuwawezesha wafungwa waliomaliza vifungo vyao kuanza maisha mapya kwa njia bora.