- 348 viewsDuration: 1:37Wakfu wa Bwosi ulitoa zawadi za krismasi kwa watu zaidi ya 2,000 wakiwemo wenye ulemavu, wajane pamoja na wananchi wasiojiweza kutoka mpaka wa Nandi na Hamisi . Waandalizi wa hafla hiyo walisema lengo kuu lilikuwa ni kufikisha ujumbe wa matumaini, mshikamano na kujali jamii, hasa makundi yaliyo hatarini kwa kuwapa chakula na bidhaa nyingine za kukithi mahitaji ya msingi.