Skip to main content
Skip to main content

Kifo cha Saif al-Islam Gaddafi kinamaanisha nini?

  • | BBC Swahili
    14,339 views
    Duration: 43s
    Saif al-Islam Gaddafi, mtoto wa kiume wa aliyekuwa kiongozi wa zamani wa Libya, Muammar Gaddafi, ameuawa katika mji wa magharibi wa Zintan. Watu wanne wasiojulikana walivamia makazi yake siku ya jumanne na kumpiga risasi na kuharibu kamera za CCTV. Mamlaka magharibi mwa Libya zimeanzisha uchunguzi ijapokuwa hakuna kundi ambalo limejitokeza kusema limehusika. Saif aliyekuwa na umri wa miaka 53 kwa miaka mingi alionekana kama mrithi wa kisiasa wa baba yake. Kifo chake kinamaanisha nini kwa mustakabali wa kisiasa wa Libya? Kwa mengi zaidi, jiunge naye @midababirye katika Dira ya Dunia TV leo saa tatu usiku kupitia ukurasa wetu wa YouTube wa BBC Swahili. #bbcswahili #Libya #Gaddafi Subscribe kupata video motomoto kila siku kutoka BBC Idhaa ya Kiswahili https://www.youtube.com/channel/UCoerKKIKIMlDYaVFSTlsWGw