Skip to main content
Skip to main content

Lori la masafa marefu lapoteza mwelekeo na kusababisha vifo vya watu 14 webuye

  • | Citizen TV
    14,585 views
    Duration: 2:13
    Watu 14 wameaga dunia katika ajali iliyotokea katika eneo la Malaha kwenye barabara kuu ya kutoka Kitale kuelekea Webuye Baada ya lori kupoteza mwelekeo na kuwagonga watu waliokuwa wakijaribu kuwasaidia majeruhi wa ajali ya awali iliyohusisha pikipiki. Kulingana na walioshuhudia ajali hiyo, pikipiki iliyokuwa ikitoka Lugulu kuelekea kakamega ilimgonga mpita njia na kumuuwa papo hapo kabla ya trela iliyokuwa ikiendeshwa kwa mwendo wa Kasi kuwagonga waliokuwa wakishuhudia tukio la kwanza. OCPD wa Webuye Rodgers Bosire amethibitisha ajali hiyo na kusema kuwa maelezo kamili kuwahusu waathiriwa yatatolewa baadaye.