Maimamu kutoka eneo la Magharibi wamenishinikiza umuhimu wa mabadiliko katika Baraza Kuu la Waislamu Nchini (SUPKEM), wakilalamikia kile wanachokitaja kama uongozi usio na uwazi na mgawanyiko unaoendelea.
Wakizungumza katika kongamano la maimamU na wahubiri kutoka magharibi mwa Kenya lililofanyika katika msikiti wa Jamia mjini Malaba kaunti ya Busia, viongozi hao wametaka baadhi ya wasimamizi wa SUPKEM kuondolewa na nafasi zao kujazwa na wajumbe wapya. Wakiongozwa na Mwenyekiti wa CIPK kaunti ya Busia Sheikh Ramadhan Musa, wamesikitika kuwa hali ilivyo sasa iliyojawa na dosari na ubadhirifu wa fedha inazua migawanyiko miongoni mwa waisilamu nchini...