- 16,488 viewsDuration: 2:57Sekta ya boda boda nchini sasa itakuwa inadhibitiwa na sheria kali, ikiwemo usajili mpya unaoonyesha maeneo maalum ya vituo pamoja na sare za rangi tofauti kulingana na maeneo wanayohudumu. Hatua hizi zinalenga kukabiliana na kuongezeka kwa visa vya uhalifu na uteketezaji wa magari ya watu binafsi na wanaboda boda. Kila kituo pia kitahitajika kuwa na mwenyekiti ambaye atawajibika na kukamatwa tukio likitokea eneo hilo likihusisha wanaboda boda.