- 216 viewsDuration: 1:32Halmashauri ya maendeleo ya serikali za mataifa IGAD imeanzisha awamu ya pili ya mafunzo ya uongozi kwa vijana katika mataifa wanachama hapa jijini nairobi. Akizungumza Kwenye hafla ya uzinduzi wa mpango huo unaofadhiliwa na serikali ya Japan katika chuo cha mafunzo ya wafanyakazi wa serikali eneo la kabete, rais wa kituo cha mafunzo ya uongozi cha IGAD daktari Simon Nyambura alisema kwamba wanalenga kuwapa mafunzo vijana zaidi ya 70 mwaka huu.