- 2,443 viewsDuration: 2:02Maafisa wa elimu mjini Narok wamefunga shule ya msingi ya Seventh Day Adventist na Sekondari msingi baada ya mwanafunzi mmoja wa kiume kuuawa katika njia tatanishi. Maeneo kadhaa ambapo mwendazake anadaiwa kukumbana na mauti yake yalikuwa na madoa ya damu hasa katika vyoo vya wavulana shuleni humo aalimopatikana amefariki. akiongea katika shule hiyo , mkurugenzi mkuu wa elimu Kaunti ya Narok Apollo Apuko amewarai wazazi kuipa muda serikali inapoendelea na uchunguzi. Mwili wa marehemu umehifadhiwa katika makafani ya hospitali ya Rufaa ya level 5 mjini Narok.