4,471 views
Duration: 55s
Afisa wa polisi anayesimamia silaha katika kituo cha polisi cha central Fredrick Okapesi amepuza madai ya njama ya kufichwa kwa taarifa katika rejesta ya bunduki inayohusishwa na kifo cha Rex Masai
Okapesi, Ameeleza mahakama kuwa tofauti zilizopo kwenye daftari zilifanyika kimakosa ila si njama ya kuficha ukweli. Akitoa ushahidi , afisa huyo alikiri kuwa sajili hiyo ina dosari, akieleza kuwa taratibu za kawaida za marekebisho, kama kupiga mstari juu ya makosa au kutumia wino kufunika, zinaruhusiwa iwapo kosa limetokea. Masai alifariki tarehe 20 Juni baada ya kupigwa risasi na polisi wakati wa maandamano yaliyofanyika jijini Nairobi, tukio ambalo limezua maswali mengi na wito wa uwajibikaji.