Skip to main content
Skip to main content

Serikali yatakiwa kukarabati mabomba ya maji makuukuu eneo la Oloitotok

  • | Citizen TV
    358 views
    Duration: 1:29
    Wito unazidi kutolewa kwa serikali kukarabati mabomba ya kusambaza maji kutoka chemichemi za Nolturesha huko Loitokitoka kaunti ya Kajiado ili kuongeza usambazaji wa bidhaa hiyo muhimu. Kampuni ya kusambaza maji katika eneo hilo inasema licha ya uwezo wa chemichemi hiyo kuzalisha lita millini 30 za maji kila siku, kampuni hiyo ina uwezo wa kusambaza lita million 12 pekee, kupitia kwa mabomba ambayo yalijengwa miaka zaidi ya 30 iliyopita ambayo hayawezi kutosheleza idadi ya watu inayoendelea kuongezeka Loitokitok.