- 828 viewsDuration: 3:20Taharuki imetanda mjini Kitale, baada ya Kamati ya Usalama ya Kaunti ya Trans Nzoia kutaja majina ya washukiwa 57 wanaotafutwa na polisi kwa tuhuma za kuhusika na wizi wa kimabavu katika maeneo ya Matisi na Tuwan. Magenge haya yamekuwa yakizunguka mitaani yakiwa na mapanga na silaha butu, yakipora mali na kutisha wakazi kwa zaidi ya wiki mbili sasa.