Skip to main content
Skip to main content

Bab al-Mandab :Iran inatishia kufunga mlango mwingine wa bahari

  • | BBC Swahili
    98,751 views
    Duration: 1:52
    🚢 Bab al-Mandab, ni moja ya njia za baharini iliyo na shughuli nyingi zaidi duniani. Mlango wa bahari wa Bab al-Mandab Strait unaunganisha Ghuba ya Aden na Bahari Nyekundu, kisha kuelekea Suez na Bahari ya Mediterania. Iran imetoa vitisho wakati huo huo, kundi la Houthis linaloungwa mkono na Iran nchini Yemen, tayari limewahi kushambulia meli katika eneo hilo na limesema liko tayari kufanya hivyo tena. Mlango mwingine muhimu, Strait of Hormuz, ambao tayari umeathiriwa sana na vita, husafirisha takribani asilimia 20 ya mafuta yote duniani. Iwapo Bab al-Mandab Strait pia utafungwa, basi karibu asilimia 12 ya mtiririko wa mafuta duniani utaathirika. Hii inaonyesha jinsi maeneo haya mawili yalivyo muhimu kwa biashara ya kimataifa na usalama wa nishati duniani. - - #bbcswahili #iran #Israel #marekani #mafuta Subscribe kupata video motomoto kila siku kutoka BBC Idhaa ya Kiswahili https://www.youtube.com/channel/UCoerKKIKIMlDYaVFSTlsWGw