Skip to main content
Skip to main content

DCI yamsaka mwajiri wa yaya aliyeuawa Kasarani

  • | Citizen TV
    6,775 views
    Duration: 2:55
    Maafisa wa upelelezi kutoka kituo cha Directorate of Criminal Investigations Kasarani wanamsaka mwajiri wa Susan Wanjiku Nyambura, yaya mwenye umri wa miaka 35 aliyeuawa kati ya tarehe 11 na 12 Mei mwaka huu, siku mbili tu baada ya kuajiriwa katika mtaa wa Ceiko, Kasarani. Familia yake ilipata habari za kifo chake baada ya maafisa wa DCI katika makafani ya City kuwasiliana nao kuhusu mwili uliokuwa umehifadhiwa humo. Mshukiwa bado yuko mafichoni huku ripoti ya uchunguzi wa maiti zikionyesha Susan alifariki kutokana na jeraha la kichwa lililosababishwa na kifaa butu.