Skip to main content
Skip to main content

Duale asema serikali itazingatia amri ya mahakama kuhusu karantini ya Ebola

  • | Citizen TV
    734 views
    Duration: 3:33
    Waziri wa Afya Aden Duale amepuuzilia mbali madai ya kuendelea kwa ujenzi wa kituo cha karantini ya Ebola kwa raia wa Marekani huko Laikipia, akisema kuwa serikali imetii amri ya mahakama ya kusitisha ujenzi wa kituo hicho. Duale hata hivyo ameonya kuwa iwapo maambukizi yataripotiwa humu nchini, hatasita kutekeleza sheria ya afya ya umma inayompa mamlaka ya kuchukua hatua zote za kuzuia kuenea kwa ugonjwa huo, ikiwa ni pamoja na ujenzi wa vituo vya karantini. Ugonjwa huo unaendelea kusambaa katika Democratic Republic of the Congo na Uganda huku jumla ya watu 138 wakiripotiwa kufariki.