Skip to main content
Skip to main content

Eliud Lagat aonya dhidi ya vurugu za maadhimisho ya Juni 25

  • | Citizen TV
    2,878 views
    Duration: 1:07
    Naibu Inspekta Jenerali wa Polisi Eliud Lagat amewaonya vijana dhidi ya kuzua vurugu na rabsha wanapopanga kuadhimisha kumbukumbu ya Juni 25 Alhamisi ijayo. Lagat amesema polisi watachukua hatua kali dhidi ya wote watakaohusika na fujo wakati wa maadhimisho ya maandamano ya Gen Z. Akizungumza mjini Mombasa, Lagat amesisitiza kuwa vijana wana haki ya kujieleza kwa amani lakini hawapaswi kutumia haki hiyo kusababisha vurugu, kutatiza amani au kuharibu mali. Aidha ameahidi kuwa polisi wataendelea kuyakabili makundi ya wahuni yanayoibuka na kuhatarisha usalama nchini.