Skip to main content
Skip to main content

Familia mbili Nairobi zataka haki baada ya vifo vya wanaume wawili

  • | Citizen TV
    2,534 views
    Duration: 1:45
    Familia mbili hapa Nairobi zinalilia haki baada ya wanaume wao kufariki kwa njia tata wakati wa mikutano ya kisiasa ya Linda Mwananchi hapo jana. Brandon Ong’or na Joseph Shikuku wanadaiwa kuvamiwa na watu wasiojulikana na kudhulumiwa kabla ya miili yao kufikishwa katika makafani ya Nairobi. Rafiki wa Shikuku anadai walivamiwa eneo la Donholm walipokuwa wakielekea katikati mwa jiji kujiunga na msafara, kabla ya rafiki yake kurushwa chini ya daraja. Ong’or pia anadaiwa kuvamiwa, huku mwili wake ukipatikana katika makafani ya Nairobi.