- 2,631 viewsDuration: 3:05Baadhi ya jamaa za waathiriwa wa mauaji ya Shakahola sasa wanataka maafisa wa polisi na hata machifu waliohudumu eneo hilo kushtakiwa na kuchukuliwa hatua. Jamaa hawa wakisema kuwa kifungo cha kiongozi wa dini potofu Shakahola Paul Mackenzie ni ya kuridhisha, bado kuna wale wanaostahiki kubeba msalaba zaidi kwa kutelekeza kazi zao mauaji hayo yalipokuwa yakiendelea. Haya yanajiri huku Waziri wa Usalama Kipchumba Murkomen akiahidi kupambana na makundi ya dini potofu, kama Ben Kirui anavyoripoti.