Skip to main content
Skip to main content

Fursa za chakula taka

  • | BBC Swahili
    9,482 views
    Duration: 1:01
    Tarehe 30 mwezi march kila mwaka ni siku ya kimataifa ya taka sifuri ikiwa na lengo la kuelimisha Jamii jinsi ya kubadilisha taka sambamba na kuzigeuza kuwa fursa kwa kuzitenga kuanzia zinapozalishwa ili wachakataji wazirejeleze au kuzalisha bidhaa nyingine zitokanazo za taka. Maadhimisho ya mwaka huu yanaangazia katika upotevu wa chakula, kwani kwa mujibu wa takwimu taka za chakula zinazalisha wastani wa asilimia 8 mpaka 10 hewa chafuzi ambazo zinapelekea uharibifu wa tabaka la ozoni. Nchini Tanzania Baraza la Taifa la Hifadhi na Usimamizi wa Mazingira (NEMC), linaadhimisha siku hii kwa maeonesho ya siku tatu mfululizo kwenye viwanja vya mnazi mmoja jijini Dar es salaam ambapo wadau mbalimbali wa mazingira wanaonesha ni namna gani taka zinavyogeuzwa kuwa fursa kuanzia uzalishaji wa wadudu kwa ajili ya malisho ya mfugo, mapambo nguo na bidhaa vyingine nyingi. Mwandishi wa BBC @eagansalla_gifted_sounds ametuandalia taarifa ifuatayo - - #bbcswahili #mazingira #fursa #vijana #takataka Subscribe kupata video motomoto kila siku kutoka BBC Idhaa ya Kiswahili https://www.youtube.com/channel/UCoerKKIKIMlDYaVFSTlsWGw