- 38,617 viewsDuration: 2:12Kinara wa DCP Rigathi Gachagua sasa anasema ni muda tu kabla ya Kiongozi wa Wengi Bungeni Kimani Ichung’wah kutemwa serikalini, kwa kushindwa kugawa kura za eneo la Kati. Gachagua sasa akidai kuwa Ichung’wah alipewa jukumu hilo na Rais William Ruto. Akizungumza kanisani eneo bunge la Kikuyu, Gachagua amemzomea Ichung’wah, huku pia akiwaonya wandani wa Rais dhidi ya kumtongoza kisiasa Kinara wa Wiper Kalonzo Musyoka.