- 6,115 viewsDuration: 2:08Hali ya kibinadamu katika kambi za wakimbizi nchini Burundi inaendelea kuzorota kufuatia ongezeko la wakimbizi wanaokimbia mapigano nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo. Kwa mujibu wa Umoja wa Mataifa, zaidi ya wakimbizi laki moja wameingia nchini humo tangu mapema mwezi Desemba, hali iliyozidi kulemea rasilimali za ndani. Mashirika ya misaada yanaonya kuwa shinikizo la kibinadamu linaongezeka, huku kambi nyingi za wakimbizi na vituo vya mpito vikikabiliwa na mzigo mkubwa katika huduma za afya, maji na usafi wa mazingira. Mwandishi wa BBC @sammyawami anaripoti. Subscribe kupata video motomoto kila siku kutoka BBC Idhaa ya Kiswahili https://www.youtube.com/channel/UCoerKKIKIMlDYaVFSTlsWGw