- 4,881 viewsDuration: 3:05Hofu imeendelea kutanda katika mpaka wa Kenya na Ethiopia, eneo la Moyale, kufuatia mapigano yanayoendelea upande wa Ethiopia kati ya wapiganaji wa jamii za Oromo na Somali. Serikali ya Kenya imethibitisha kifo cha raia mmoja, ingawa wenyeji wanaripoti kuwa idadi ya waliofariki huenda ni kubwa zaidi. Wakati huohuo, idadi ya wakimbizi wanaotafuta usalama nchini Kenya imefikia elfu 50. Inspekta Jenerali wa Polisi, katika ziara yake Moyale, amewahakikishia wenyeji usalama huku serikali ikiendelea kutafuta suluhu ya kukomesha mapigano hayo.