- 17,022 viewsDuration: 2:56Hofu imeendelea kutanda katika mpaka wa Kenya na Ethiopia eneo la Moyale, kufuatia vita vinavyoendelea upande wa Ethiopia kati ya wapiganaji wa jamii ya Oromia na Somali. Serikali ya Kenya imethibitisha raia mmoja kufariki japo idadi inaripotiwa kuwa juu kulingana na wenyeji. Idadi ya wakimbizi wanaotafuta usalama nchini ikifikia elfu hamsini. Inspekta Jenerali wa polisi katika ziara yake Moyale amewahakikishia wenyeji usalama serikali ikitafuta suluhu ya kukomesha vita hivyo.