Skip to main content
Skip to main content

IEBC yaonya wanasiasa kuhusu uchochezi kuelekea uchaguzi wa 2027

  • | Citizen TV
    520 views
    Duration: 1:29
    Tume Huru ya Uchaguzi na Mipaka (IEBC) imeonya kuwa wanasiasa watakaopatikana na hatia ya uchochezi watachukuliwa hatua na huenda wakazuiwa kushiriki Uchaguzi Mkuu ujao. Katika hafla ya kuzindua taratibu za uchaguzi wa mwaka ujao, idara ya usalama pia imeahidi kutumia nguvu zote za kisheria kuwawasilisha watakaokiuka sheria kwa IEBC ili wasiwaniwe kugombea viti katika Uchaguzi Mkuu wa 2027.