- 375 viewsDuration: 2:33Mwenyekiti wa tume ya uchaguzi IEBC Erastus Ethekon amesema kwamba tume hiyo itawapiga marufuku wanasiasa na wawaniaji wa nyadhifa mbali mbali, watakaopatikana na hatia ya kuzua ghasia na fujo wakati wa kampeni za uchaguzi. Akizungumza katika mkutano kuhusu maandalizi ya usalama wa uchaguzi mkuu ujao jijiji Nairobi, Ethekon alitangaza kwamba ukosefu wa vitambulisho miongoni mwa Wakenya ni changamoto kuu katika usajili wa wapiga kura nchini. Mkutano huo pia ulihudhuriwa na waziri wa usalama Kipchumba Murkomen