- 3,435 viewsDuration: 1:42Mustakabali wa Rais wa FIFA, Gianni Infantino, umeendelea kuwa gumzo duniani baada ya kuitisha kikao cha dharura mjini Rabat, Morocco, wakati shinikizo la kumtaka ajiuzulu likizidi kuongezeka. Shinikizo hilo linahusishwa na mpango wake wenye utata wa kuuza sehemu ya biashara ya Kombe la Dunia kwa wawekezaji binafsi. Wakati mjadala huo ukiendelea, majina ya viongozi kadhaa mashuhuri wa soka duniani tayari yameanza kutajwa kama wanaoweza kumrithi endapo ataondoka madarakani. Mwandishi wa BBC @loko_omi anatueleza zaidi. 🎥: @frankmavura Subscribe kupata video motomoto kila siku kutoka BBC Idhaa ya Kiswahili https://www.youtube.com/channel/UCoerKKIKIMlDYaVFSTlsWGw